BLOGU YA MWAFRIKA

Pages

  • MWANZO
  • Siasa na Jamii
  • UCHAGUZI
  • MACHAPISHO
  • WASILIANA NASI
  • KUHUSU SISI
  • Makala na Hotuba
  • Michezo na Burudani

Saturday, 1 February 2014

MGEJA AWAPASHA MALECELA na MAKONDA.....pata story zaidi

 

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARITAREHE 1
    FEBRUARI 2014

    MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE
    RADHI KWA VIONGOZI WA DINI

    0.1 Kitendo alichokifanya hivi karibuni Ndugu Paul
    Makonda Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji pale
    alipoongea na vyombo vya Habari pamoja na mambo
    mengi aliyoyaongea kubwa zaidi ni alipotamka wazi
    kwa kuwatuhumu baadhi ya Viongozi wa Dini kwa
    kutoa maneno ya kejeri na dharau dhidi yao kuwa
    “MASHEIKH NA MAASKOFU WAKIWEMO NA VIJANA
    WANAOTAKA FEDHA ZA BURE WAENDE KWA EDWARD
    LOWASA” kitendo ambacho hakuwatendea haki wala
    adabu Viongozi hawa wa Dini.
    Kitendo hicho cha kuwakejeri na kuwadhalilisha ni
    utovu wa Nidhamu wa hali ya juu sana, kwani kauli
    aliyoitoa kila Muumini ilimshitua sana, kwani ni kauli
    haikupaswa kutolewa na Kiongozi wa Vijana
    aliyekuwa katika nafasi Muhimu ya Uongozi wa
    Jumuiya Kitaifa, kwani kauli yake hiyo yenye ukakasi
    wa hali ya juu sana imempa kichefuchefu kila mmoja
    anaewaheshimu Viongozi wa Dini, kwani Viongozi wa
    Dini wanaheshima zao binafsi na kuheshimika
    Duniani kote na mpaka Serikali huwaomba Viongozi
    wa Dini kushiriki pamoja kutatua na kushauriana
    katika maswala mbalimbali yanayoizunguka jamii.
    Kauli hiyo ni nzito sana aliyoitoa Ndugu Paul
    Makonda sio ya kuipuuza hata kidogo na kuicha hivi
    hivi nina muomba kwa Heshima na taadhima
    Mwenyekiti wa Vijana wa Taifa awathibitishie
    Watanzania kuwa kauli aliyoitoa Ndugu Paul
    Makonda ni ya Umoja wa Vijana au ni yake binafsi.
    Kwani mimi binafsi nimekuwa katika Umoja wa
    Vijana kama Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa
    Shinyanga mstaafu na Mjumbe wa Baraza Kuu la
    Umoja wa Vijana Taifa lakini pia Mjumbe wa Kamati
    ya Utekelezaji Umoja wa Vijana Taifa, nafahamu kauli
    au matamko mazito kama yaliyotolewa na Ndugu
    Paul Makonda hutolewa na Mkutano mkuu wa Taifa,
    Mkutano wa Baraza Kuu Taifa na hata kamati ya
    Utekelezaji Taifa.Mimi siamini kama hiyo ni Kauli ya
    Umoja wa Vijana kwa kadri ninavyofahamu utaratibu
    ndani ya Jumuiya na Chama kwa ujumla, sasa
    tunajiuliza huyu kijana kauli hizi nzito nzito ambazo
    hazilingani na umri wake na wala hadhi ya kiuongozi
    aliyonayo anazitowa wapi huenda tunaamini kuna
    kundi au genge la mahafidhina liko nyuma yake
    lililoamua kumtumia aidha kwa kujua au kwa
    kutokujua.

    Jambo jingine muhimu alitutuhumu pia sisi yani
    mimi Khamis Mgeja, Mzee Mgana Msindai na Ndugu
    John Guninita kuwa alidai t--------- na Ndugu Edward
    Lowasa, tuhuma hizi si za kweli hata kidogo napenda
    Watanzania wafahamu tuhuma zote mbali mbali
    ambazo kijana huyu amekuwa akitushutumu si za
    kweli na ni za kipuuzi ninaiomba jamii kumpuuza
    kwani Ndugu Makonda bado mchanga kisiasa
    anatafuta umaarufu kwa kasi kwa kutumia migongo
    yetu sisi wakongwe kisiasa, kwani sisi aliotutuhumu
    atambue sisi ni wakongwe na ni Magwiji katika siasa
    za kiungwana hapa Tanzania, tunauwezo wetu
    binafsi wa kufikiri na kuamua kile tunachokiamini
    kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla, kwa
    ujumla tunataka Ndugu Paul Makonda na washirika
    wake waache kelele ambazo wamekuwa
    wakilalamika mara kwa mara hii ni dalili ya
    kuelemewa ndio maana hawaishi kumsemasema na
    kumkejeri Ndugu Edward Lowasa wakati ambapo
    jamii inamuona kuwa ni mtu wa msaada mkubwa
    katika kuchagiza maendeleo kwa kushirikiana na
    jamii. Kijana Makonda atambue sisi tumewekeza
    jasho jingi katika chama hiki na kamwe hatutokubali
    kudhalilishwa na kijana mchanga wa kisiasa kama
    huyu, pia kama ni kuwekeza jasho sisi tuna debe
    ishirini yeye hata robo hajafikisha katika medani za
    kisiasa kwa hivyo anafanya maajabu ya kisiasa ni
    maajabu ya panya kufukuza paka na anacheza
    ngoma asiyoijuwa.Pia jamii inamuona Ndugu Edward
    Lowasa ni mtu muungwana, mwenye uwezo mkubwa
    wa kiutendaji, mwenye ushauri na ushawishi
    mkubwa katika machangizo ya maendeleo, sifa
    kubwa nyingine ya ziada ni uvumilivu na hasa
    kuwavumilia watu wenye kumrushia madongo kama
    Paul Makonda na genge lao la mahifidhina.
    Kuhusu kauli aliyoitamka Ndugu Makonda ya
    kwamba Ndugu Edward Lowasa hawezi kuwa Rais
    kauli hii imetoa picha ya kuyajuwa yaliyofichika
    katika fikra za kundi hili la wahifidhina lakini pia
    watambue maamuzi yote hufanywa na Vikao halali
    vya chama na jumuiya zake, na wakati ukifika vikao
    vitaamua na si Makonda na marafiki zake.
    0.2 MZEE MALECELA KUPONGEZA KAULI ZA KASHFA
    DHIHAKA NA KEJERI DHIDI YA VIONGOZI WA DINI
    Kufutia tukio la hivi karibuni la kijana Paul Makonda
    kutoa maneno ya kashfa kejeri na dhihaka dhidi ya
    viongozi wa Dini, baadhi ya wanasiasa na vijana
    maaajabu makubwa kutokana na kauli hizo za
    Makonda tumemshangaa Mzee Malecela kuibuka na
    kuunga mkono na kumpongeza kijana huyu mtovu
    wa nidhamu.
    Tulitegemea kila Mtanzania kwamba baada ya kauli
    hizo Mzee Malecela angeibuka na kumuongoza njia
    sahihi na kumpa ushauri kijana huyu aliyepotea
    kimaadili wa kwenda kuwaomba radhi na
    kuwaangukia viongozi wa Dini, ndugu Edward
    Lowasa, Ndugu Khamis Mgeja, Ndugu Mgana
    Msindai, Ndugu John Guninita ikiwemo na vijana kwa
    ujumla.Maajabu makubwa jambo ambalo
    Watanzania hawakutegemea jinsi wanavyomfahamu
    Mzee Samwel Malecela na heshima yake, tulitaraji
    kuwa Mzee angemkemea kijana huyu mtovu wa
    Nidhamu badala yake anampongeza na kumuunga
    mkono na kuwataka Watanzania wamuunge mkono
    kwa kauli zake za utovu wa Nidhamu ambazo hazina
    tija kwa Chama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla,
    pia katika maajabu mengine Mzee Malecela
    alimshambulia mwanachama mwenzake Ndugu
    Edward Lowasa kwa kumtuhumu kwa tuhuma nyingi
    mbalimbali ambazo hana ushahidi nazo.Mzee
    Malecela amesahau huko nyuma yeye alishawahi
    kutuhumiwa kuwa alipewa fedha kutoka nchi za
    uarabuni na mpaka kubadilisha dini na kuitwa jina la
    JUMANNE ili aungwe mkono kupewa nguvu za
    kugombea Urais.
    Kuhusu uchu wa Urais anaomtuhumu Ndugu Lowasa
    amesahau yeye ndiye ana uchu mkubwa sana wa
    Madaraka alikuwa akiomba nafasi za ndani ya
    Chama haswa kwa kiti cha Urais kwa awamu
    mbalimbali akaonekana hafai na hatoshi na mpaka
    jina lake likawa halipitishwi na chama baada ya
    kumgundua ni dhaifu na anakasoro kubwa za
    kimaadili na mpaka ikapelekea Baba wa Taifa
    akachoka kumvumilia na hatimae alimtungia kitabu
    “UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA” hii ni
    kuonyesha kuwa Mzee Malecela alikuwa sugu wa
    matatizo yaliyokuwa yakikiuka maadili.Jambo jingine
    alilokuwa nalo la uchu wa madaraka Mzee Malecela
    ni pale alipong’ang’ania kiti chake cha ubunge bila
    kujali umri wake na wananchi wa jimbo la Mtera
    ilifika mahala walimchoka baada ya kugundua
    anasinzia Bungeni na kwenye jimbo laketulishuhudia
    Kibajaji kikiliangusha Katapila maana yake
    aliangushwa ubunge na mtoto mdogo Mhe
    Livingstone Lusinde.Jambo jingine Mzee Malecela
    ameshindwa kutambua wanaokivuruga chama ni
    wale wanaozungumza nje ya vikao halali vya chama
    na jumuiya zake na kuyageuza kuwa ndio msimamo
    wa chama au jumuiya.
    Kwa hivyo Mzee Malecela kuendelea kutushambulia
    hatutendei haki kwani hakuna shughuli yoyote ya
    chama iliyokwama kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa
    kwa sababu yetu sisi.NINAPENDA KUTOA USHAURI
    KWA MZEE MALECELA, MAKONDA NA WATANZANIA
    WENZANGU KWA UJUMLA, Tanzania kama taifa
    tumefika pabaya kwani kila mmoja amebaki kuwa
    mlalamikaji na kutuhumiana pasipokuwa na ushahidi
    hili jambo ni hatari kwa mustakbali wa nchi kwani
    hivi sasa baadhi ya watu wanamgeuza Ndugu
    Edward Lowasa kuwa ni agenda ya kitaifa huku
    wakiacha mambo muhimu ya nchi na maisha ya
    watanzania.kwani tulitegemea wazee wetu kama
    kina Mzee Malecela watushauri vipi taifa linaweza
    kukabiliana na changamoto zilizopo hivi sasa kwa
    mfano deni la taifa, mchakato wa Katiba Mpya,
    matatizo ya umasikini, tatizo la ajira kwa vijana,
    hombwe kubwa kuwahi kutokea baina walionacho na
    wasionacho, mauaji yanayotokea sasa maeneo
    mbalimbali kati ya wakulima na wafugaji ikiwemo
    kuchomeana nyumba, mauaji ya kikatili kule Tarime
    na maeneo mbalimbali nchini, ajali mbali mbali za
    barabarani zinazouwa nguvu kazi ya Taifa, tatizo
    kubwa la rushwa, uporaji wa rasilimali za Taifa na
    ujangili wa kutisha, Tanzania kutumika kama korido
    la kupitishia madawa ya kulevya na binadamu,
    oparasheni tokomeza, wananchi kujichukulia sheria
    mkononi, ubadhilifu wa mali za umma haswa
    ukizingatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za
    serikali na taarifa za kamati mbalimbali za bunge,
    jambo jingine kubwa lilipo kwa sasa ni kuhusu
    rasilimali ya gesi iliyovumbuliwa kwa wingi nchini
    wakati taifa lipo katika mchakato wa kutunga sera na
    sheria ya gesi na mafuta.
    Mzee Malecela na wenzake hayo yaliyotajwa hapo
    juu ndio mambo muhimu yanayogusa nchi na sio
    mtu Lowasa Lowasa Lowasa tulitegemea atushauri
    Tanzania kama taifa tufanye nini Watanzania kwa
    kushirikiana na Serikali yetu kwani matatizo hayo
    yanahitaji ushirikishwaji baina ya wananchi na
    Serikali yao, Watanzania wangeyapata hayo kupitia
    uzoefu wake kama alivyowahi kuwa Makamu wa
    Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM
    kuliko maajabu ya kuonyesha Flana yenye maneno
    ya “FRIENDS OF LOWASA” kuwa kama ndio tatizo la
    Taifa.
    Mzee Malecela kuwaonyesha Watanzania Flana ya
    Lowasa ndio tatizo la taifa hii inaonyesha wazi Mzee
    amechoka na amefilisika kifikra na anazeeka vibaya
    ninapenda nimpe ushauri wa bure Mzee wangu
    atulie alinde heshima yake.Pia napenda nitoe
    ushauri kwa Mzee Malecela, Paul Makonda pamoja
    na washirika wao wasome alama za nyakati na
    waangalie mahitaji ya siasa kwa sasa na waone
    Watanzania wanamuhitaji Kiongozi wa namna gani
    wa Tanzania ya kesho, ninawaomba wakubali yaishe
    wasije kupinganaTanzania na nguvu ya umma na
    upepo wa kisisa kwa sasa na pia watambue mpaji ni
    MUNGU alitakalo MUNGU hakuna mwanadamu
    atakaelizuia.
    NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA UJENZI WA TAIFA
    MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI
    WATANZANIA
    TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA
Posted by BLOGU YA MWAFRIKA at 05:33
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

WALIOTEMBELEA BLOG

Labels

  • makala
  • Michezo na Burudani
  • siasa na jamii
  • UCHAGUZI

About Us

  • BLOGU YA MWAFRIKA
  • Deo Kisandu
  • Unknown
  • Unknown
  • Unknown
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU

Translate

HABARI MPYA

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

  • AJIRA MPYA ZA WALIMU 2014.
    Jenista Mhagama   Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo na Ufundi Kutokana na mengi kuongelewa kuhusu ajira mpya za walimu,ambapo awali ...
  • HISTORIA KAMILI YA EXTRA MUSICA BAND inapatikana hapa
      Extra Musica ni kundi la muziki linalotoka katika nchi ya Congo Brazzaville . kundi hili lilianzishwa mwaka 1993 na wanamziki walioanzi...
  • ZITTO aibuka Kidedea Mahakamani, Wakili Kijana amuokoa ZITTO KABWE.
    Source Eatv&Jamiiforum Judge kaamua kuwa kamati haitakuwa na mamlaka ya kujadili uanachama wake mpaka atakaposikilizwa na pingamizi ...
  • POLISI AKIJA KUKUKAMATA FANYA HIVI......
    Jeshi la Polisi ni mali ya wananchi, hivyo Ulinzi shirikishi ni wa pamoja kufikia Ulinzi na Usalama wa Mtanzania. Kwakuwa Watanzania...
  • ZITTO AWAUMBUA WABUNGE KWA KUFICHA UKWELI....AANIKA KILA KITU ANACHOPATA MBUNGE KWA MWAKA NA BAADA YA MDA WAKE.
    Mbunge wa Kigoma Kasikazini almarufu kama Mwanademokrasia wa kweli leo kaanika ukweli na kuonesha uwazi wa maslahi wanayopata viongozi wetu....
KUWA WA KWANZA KUPATA MATUKIO HAPA:LIKE FACEBOOK FANS PAGE YETU HAPO CHINI
×

TAFUTA UNACHOTAKA KUSOMA

Flag Counter

MAP VISITOR

MAKTABA YETU

BLOG RAFIKI

  • LEWIS MBONDE BLOG
    BLOGU YA LEWIS MBONDE BLOG YASITISHA KUTOA MAUDHUI MTANDAONI - Kutokana na matakwa ya kisheria ya maudhiu ya kutoa huduma za kimtandao bila kuwa na leseni iliyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za mawasiliano t...
    7 years ago
  • dj sek
    PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...
    9 years ago
  • NCCR-MAGEUZI BLOG: PAMOJA TUTASHINDA!
    TAMKO LA NCCR MAGEUZI KUHUSU UFISADI WA IPTL KUPITIA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW - *TAMKO LA NCCR MAGEUZI KUHUSU UFISADI WA IPTL KUPITIA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW* UTANGULIZI Itakumbukwa na watanzania kuwa kwa takribani miezi miwili sasa w...
    11 years ago
  • BLOGU YA MWAFRIKA
    HAPAHAPA TANZANIA-MABADILIKO YA JAMII KWANZA, SIASA YA VYAMA PEMBENI. - [image: picha ya deogratius kisandu]
    11 years ago
  • JamiiForums | The Home of Great Thinkers
    -

Followers

ALL RIGHT RESERVED DESIGNED BY LEWIS MBONDE +255658194194. Simple theme. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.