Saturday 18 January 2014

KISANDU aibuka kidedea MJUMBE NEC-TAIFA NCCR-MAGEUZI.

Deogratius Kisandu akiomba kura jana Diamond jubilee
 


Uchaguzi mkuu wa jana  tarehe 18.01.2014 wa chama cha NCCR_Mageuzi ulihudhuriwa na watu wengi wakiwemo wadau wa siasa na maendeleo, kutoka CHADEMA waliwakilishwa na Mwenyekiti Taifa (Freeman Mbowe) na Katibu Mkuu (Dr.Slaa), upande wa CUF alikuja Mwenyekiti Taifa (Pro. Ibrahim Lipumba) na kwa chama tawala CCM alikuja Mwenyekiti Taifa(Mzee Mangula), pia Mzee Sabodo naye alishiriki na kutoa hotuba yake pamoja na mchango wake kwa chama cha NCCR-Mageuzi.

Nafasi zilizokuwa zinagombaniwa jana ni Mwenyekiti wa chama Taifa, makamu mwenyekiti bara na Zanzibar na nafasi zingine ni WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU(NEC).


 Upande wa nafasi ya Mwenyekiti alishinda Mh. James Mbatia akimuangusha Charles Makofila na hivyo tume kumtangaza  Mbatia kuwa mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, nafasi ya Makamu bara alishinda mama Leticia na Upande wa Makamu Zanzibar aliendelea kuwa yuleyule kwani alipita bila kupingwa Mh. Ambar.


Katika nafasi ya WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU(NEC) Deogratius Kisandu alikuwa kundi hatari ambalo lilikuwa na wagombea takribani 38 na waliokuwa wanahitajika ni Wajumbe 10 tu kutoka Tanzania bara. Japo Kisandu alipangiwa majukumu mengi ya kufanya na yaliyomfanya asipate mda wa kuomba kura lakini umakini wake ulibadilisha ukumbi na kujikuta ukishawishika na kuhamasika na hivyo kushinda na kufanikiwa kuwa MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA(NEC).

Blogu ya Mwafrika na Team nzima ilikuwa ukumbini ikifatilia mchakato mzima wa uchaguzi hivyo inawatakia kazi njema washindi wote.

1 comment:

  1. Hongera Mwl. Kisando tunategemea siasa safi toka kwako ili jamii iendelee kutuamini vijana ktk majukumu mbalimbali.

    ReplyDelete