Jenista Mhagama Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo na Ufundi |
Kutokana na mengi kuongelewa kuhusu ajira mpya za walimu,ambapo awali waheshimiwa mbalimbali wa wizara husika walikwisha kutoa matamko tofauti ambayo mpaka sasa hayajatimia,naye naibu waziri wa elimu mafunzo na ufundi mh.Jenista Muhagama aamua kunena.
Awali
mwaka jana mwishoni, Naibu waziri anayeshughulikia Elimu
(TAMISEMI),Kassim Majaliwa,alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari
na kusema ajira hizo zinategemewa kutoka mwezi wa kwanza 2014,ambapo
kauli hiyo haikutimia mpaka sasa mwezi wa pili na hakutoa tena tamko
lolote juu ya hilo.
Mwishoni
wa mwezi wa kwanza katibu wa Elimu Mafunzo na Ufundi, Prof. Sifuni
Mchome,naye alitoa taarifa kupitia kituo kimoja cha TV,yaani
EATV,akisema kila kitu tayari na wanasubiri kutangaza tu hizo ajira mpya
za walimu,ambapo mpaka sasa pia kauli hiyo bado haijatimia maana ni
kama wiki tatu zimeshapita.
Tarehe
11/02/2014,kulikuwa na kikao ambacho kilihusisha wadau mbalimbali wa
elimu yaani walimu na wadau wengine wa sekta hiyo.Kikao hicho
kiliendeshwa ndani ya ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugalo iliyopo
manispaa ya Iringa.
Kikao
hicho ambacho mgeni rasmi alikuwa mh. Jenista Mhagama kama naibu waziri
Elimu,aliweza kusikiliza mengi yanayoikumba sekta ya elimu.Pamoja na
mambo mengi yaliyozungumziwa,wadau walitaka kufahamu ajira mpya za
walimu zitatoka lini.
Kwa
mujibu wa naibu waziri huyo alisema kuwa wale wote wanaosubiri ajira
hizo,majina yatatoka tarehe 1/04/2014 kwasababu kwa sasa serikali haina
fedha na nyingi zimetumika kwenye maswala mbalimbali ya kitaifa lakini
kubwa ni maswala ya katiba mpya.
Kwa
maelezo zaidi unaweza ukawasiliana na mdau yeyote wa elimu
aliyehudhuria kikao hicho cha tarehe 11/02/2014,shule ya sekondari
Lugalo iliyopo manispaa ya Iringa mjini. habari zaidi ingia hapa:
http://tumsifu-thegreat.blogspot.com/2014/02/hatimea-mh-jenista-mhagama-anena-kuhusu.html?spref=fb
No comments:
Post a Comment