Mbunge Rechel Mashishanga-CHADEMA.
Ndugu wasomaji wa online; katika ile hali inayoitwa mazoea yana tabu yake na pia mazoea yana raha zake, Blogu ya Mwafrika inaendelea kukuletea yale yanayojiri katika jamii yetu ya kiafrika ili nawe uweze kujua na ikiwezekana uweze kujifunza na kuimarisha mfumo wako wa maisha.
Leo Blogu ya Mwafrika inamleta kwenu Mbunge wa Viti Maalum wa CHADEMA kutoka mkoa wa Shinyanga Mh. Rachel Mashishanga, amekuwa Mbunge pekee wa kike anayeshiriki na wananchi kwa namna mbalimbali katika maeneo mbalimbali na amekuwa akishirikiana na jamii katika shughuli za kijamii, hasa mkoani Shinyanga kwa kujenga Chama chake na kujenga Tanzania Mpya yenye mtazamo mpya kwa wanashinyanga.
Blogu ya Mwafrika imeona mchango wake mkubwa sana pia katika mitandao ya kijamii hasa pale anapotoa maoni yake na kujibu maoni au maswali anayoulizwa kitu ambacho wabunge wengi huweka POST kwenye mitandao na hawajibu COMENT zilizojitokeza, kitu ambacho mbunge wetu wa leo anashiriki vizuri sana.
Bi. Mashishanga ni mzawa na mkazi wa Shinyanga, hivi karibuni ameshiriki kwa karibu sana kutoa maoni yake tena kwa changamoto kubwa katika mtandao wa kijamii wa WHATSUP GROUP ndani ya JUKWAA LA SHINYANGA kitu ambacho kinamfanya aendelee kupendwa na wanachi wake kwa kuwaunganisha kuwa kitu kimoja. Blogu ya Mwafrika inampongeza Rechel Mashishanga kwa ushirikiano mkubwa anaouonesha kwa wananchi wake. Wadau wetu waliongea naye kwa mawasiliano ya simu na kumpongeza kwa moyo huo.
Mungu Ibariki Tanzania Mpya.
|
Mbunge wetu jukwaani.
|
|
No comments:
Post a Comment