Ndugu Watanzania wenzangu kumekuwepo na wimbi kubwa sasa la viongozi wengi hapa nchini nikiwemo na mimi kuutaka Urais wa
mwaka 2015, kila mmoja
amekuwa na vigezo vyake kwa maslahi yake binafsi bila kuangalia wananchi wa Tanzania wanataka nini haswa.
Kimsingi niliwahi kusema Rais ajaye anatakiwa awe hajawahi kuwa mbunge au waziri au Diwani na ndio anaweza kuwa kiongozi mzuri maana atakuwa
hana chembechembe ya kifisadi kama ilivyokuwa kwa mwl. Nyerere ambaye hakuwahi kuwa mbunge wala waziri zaidi ya uongozi ndani ya chama
chake.
Sasa leo na hili la Elimu, kutokana na kiwango cha elimu kushuka hapa nchini tatizo inaonekana kuwa na mwingiliano wa kisiasa, wanasiasa wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na watoto wao wanasoma International Schools huku sisi watoto wa wakulima
tukiumia na shule yatima za kata.
Kwa mantiki hii Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa awe ni yule aliyesoma shule zetu za kata kwani hii itasaidia kujua machungu ya Watanzania na adha ya elimu hapa Tanzania, pia
lazima awe amesoma vyuo vya hapahapa Tanzania kwani itasaidia Rais ajaye kujua matatizo ya bodi ya mikopo, migomo ya vyuo na mahitaji ya wanachuo.
Mimi kama mmoja wapo wa wanafunzi waliopitia shule hizi za kata pamoja na kufundisha shule hizi za kata na kusoma vyuo vya hapahapa Tanzania nina nafasi kubwa zaidi ya kuwa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani 97% ya wanafunzi wamesoma shule hizi na vyuo hivi na wengine bado wanasoma na ndio wapiga kura wa Rais ajaye. Haya nimaoni yangu kwa mujibu wa Katiba ya nchi Ibara ya 18.
DEOGRATIUS KISANDU
|
No comments:
Post a Comment