hivi karibuni Zitto aliandika katika ukurasa wake wa facebook maneno ya liyoonekana kuwagusa hasa watu waliokatika ndoa, kipengele cha mwisho wa maneno yake "Mtu ambaye hawezi kumheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kumnyooshea mtu kidole kuhusu maadili"
Wapo kina dada ambao kwenye mitandao wa facebook wameonekana kuipenda kauli hiyo Olivia Sanare ambaye katika ukurasa wake kaandika hivi "Mtu ambaye hawezi kumheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kumnyooshea mtu kidole kuhusu maadili"by zitto kabwe.
Hata hivy mtangazaji wa kipindi cha wanawake Live naye ameonekana kuguswa na kauli hiyo,,,,ona alivyofunguka hapa:
Hiyo inaitwa Vunja Ukimya, Elimika,
Uaminifu wa Kiongozi yeyote na dhamira yake ya kubeba Dhamana ya Matumaini ya Wananchi Ni Lazima Ianzie nyumbani kwake.
Kama Kiongozi ameshindwa kutunza Uaminifu kwa Mke wake, (familia moja) atawezaje kwa jamii (familia lukuki) kama Kiongozi ameiumiza familia yake ya watu wachache, atashindwa vipi kuwaumiza watanzania wengi asiowajua....
Unapomuumiza Mke wako aliyekuzalia Watoto, kwa kutoka nje ya Ndoa, tena Ukazaa huko!! wewe huna tofauti na Mafisadi wengine..............
Hufai Kuwa Kiongozi hata wa Nyumba 10.........
B
Huo ndo msimamo wangu mimi Joyce Kiria..... Tokeni povu lakini hamnisumbui ng'o... Ukweli daima nitasema ili niepuke Unafiki na Uzandiki niwe Huru..........
TAKE: Japo hakuna kiongozi yoyote aliyetajwa ila ni mhimu sana kujifunza wanandoa kuheshimiana japo ndoa zinachangamoto nyingi sana hasa ukiwa hujaoa au kuolewa ni vigumu kujua changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment