Monday, 17 February 2014

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE AMWAGIA SIFA RAIS KAGAME.

"Nilikutana na Rais Kagame 2011 Ikulu ya Rwanda. Nilijifunza mambo mengi kwake hasa kwenye Uongozi.

Moja kubwa ni ku-control media. Wanahabari wa leo wanahitaji habari zilizo chujwa toka kwa kiongozi mkuu vinginevyo watalivuruga Taifa.

Ikulu ya Rwanda wanao chukua habari ni watu maalum wa Rais Kagame, wakisha chuja ndo wanakuletea. Hata sisi walipiga picha zote, kisha wakatuma wao tena kwenye Email yangu tu.

Ndo maana hata siku moja huwezi kupata picha ya Rais Kagame kasinzia wala kauli yoyote yenye utata haiwezi kuifikia jamii. Lazima tukumbuke kuwa kiongozi pia ni binadamu!

Wahenga waliwahi kusema, Uhuru bila sheria ni sawa na fujo pia sheria bila uhuru ni sawa na utumwa.

Labda tuutafakari utaratibu huu!" ameandika Mrisho Gambo mkuu wa wilaya ya Korogwe.


hABARI ZAIDI INGIA KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK: https://www.facebook.com/mrisho

No comments:

Post a Comment