Naomba nitoe mrejesho katika masuala ndani ya jimbo letu la Ubungo;
1. Barabara ya Goba-Mbezi Louis nawaomba wananchi wenzangu mfuatilie
matengenezo yaliyoanza na kutoa mrejesho; lami kidogo nayo itaanza.
Tuungane kupendekeza nyongeza bajeti hii
2. Barabara ya
Malambamawili-Msigani naombeni tathmini ya matengenezo yaliyofanyika;
ujenzi wa lami utaanzia kipande cha Kinyerezi-Kifuru. Kwa hii sasa ni
hatua.
3. Barabara ya Bonyokwa-Mavurunza Kimara mwisho; nimewasiliana na Manispaa ya Kinondoni kukumbusha utekelezaji wa ahadi ya matengenezo. Majibu kesho.
4. Barabara ya Matete-Jeshini-Golani haikutengewa fedha KMC, nimewatumia ujumbe TANROADS wakishughilikia Msewe wasogee
5. Barabara ya Mavurunza-Golani-Msewe-Matete hali ya barabara ni tete.
Nimewasiliana na diwani Pascal Manota na kumtumia posho ya leo kuweka
mafuta grader. Ikiwa unatumia barabara za Mavurunza-Golani-Matete
wasiliana na Diwani 0713792966 utuunge mkono sasa; mamlaka zingine nazo
tunazifuatilia
Tayari nimefika Dodoma, nimekabidhiwa makabrasha; kesho Bunge Maalum. Ingia http://www.katiba.go.tz soma nyaraka tujadiliane tupate katiba bora
Kwa namna ya kipekee nawakatika kila la kheri wahariri walioteuliwa na
gazeti la MWANANCHI (Ndugu Sanga na Ndugu Miruko). Naamini mtazingatia
ADUUU na kulinda uhuru na uwajibikaji wa uhariri.
habari zaidi: https://www.facebook.com/john.mnyika
No comments:
Post a Comment