Monday, 17 February 2014

Namna ya kuamini kitu sahihi

Natanguliza salmu zangu za upendo kwa wote hasa vijana wenzangu;rafiki na ndugu zangu,Mama na Baba ,Dada kaka na wadogo zangu.

 

Namshuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kutafakali pamoja mambo sahihi ya kufanyia kazi tunaposoma waraka huu na nyaraka nyingine Sahihi.

 

Katika mambo yote ambayo tunayatia mikono kwa manufaa au katika namna yoyote ile chini ya jua hufanyika kutokana na kuamini katika matokeo fulani.

 

Kuamini,huambatana na kuwa na hali ya ufahamu juu ya jambo fulani;katika namna rahisi ndio kukua kiakili.

 

Kukua kiakili sio kujua sio kujua uzinzi,uongo na tabia nyingine mbaya zinazofanana na hizo;bali ni kupata ufahamu na maarifa sahihi ya kuishi na kutembea katika jambo na wakati fulani.

 

Kuna namna mbali mbali ambazo ni utaratibu wa kujifunza usahihi:

1.Maamuzi au mazoea ya mtu binafsi katika namna ya kupata uhitaji

2.Maamuzi au mazoea ya kundi fulani la watu katika jamii katika namna fulani ya kupata uhitaji

3.Mwenyezi Mungu ambaye aliyetuumba naye ana namna ambavyo anapenda kila mmoja awe.

 

Katika yote hayo ni bora kupata usahihi unaotokana na Mungu ili kuishi yaani kutembea katika jambo fulani na wakati fulani.Usahihi huu au ufahamu na maarifa haya yanapatikana katika vitabu vitakatifu vinavyovyozungumza uwepo wa Mungu mmoja anayefanya kazi katika namna tofauti,na kumpa kitu chema mwanadamu kinachotokana na neno lake mwenyewe.Kwa hiyo ili kupata uhitaji wowote katika usahihi ni lazima kumcha Mungu.

 

Kumcha Mungu katika jamii ya sasa ndio namna pekee ya kutuwezesha vijana kushinda ulimwengu;kutambua majukumu yetu ya kijinsia ambayo Mungu ametupa na kupinga;usagaji na uhuru wa mabo ya kike na yale mengine yote ya kijinsia ambayo hayampi Mungu utukufu kama ushoga katika nafi zetu,kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tuna pinga hira za shetani.

 

Mfano unaotokana na Tukio la karibu;1.Valentine.Kuna namna ambavyo tunasherehekea valentine kwa kuhamasisha mahusiano ya kingono,jambo hili linaleta laana kwa jamii fulani au taifa. 

mwanzo6:1-6

"1.Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao.

2 wana wa Mungu walipowaona hao binti za wanadamu ni wazuri,wakajitwalia wake wowote waliowachagua.3.Bwana akasema roho yangu haitashindana na Mwanadamu milele kwa kuwa naye ni nyama;basi siku zake zitakuwa miaka mia ishirini........."

 

Tukiendelea kusoma na kutafakali vizuri,tunatambua ya kwamba nguvu ya maamuzi ya mahusiano kati ya Mwanamume na mwanamke pia inatoka kwa Mungu,na neema ya Mungu pekee ndio inayotuongoza baada ya kufanya maamuzi kinyume na hayo,vinginevyo ni laana.

 

Tukiendelea mbele tunajifunza kuwa Mungu alichukizwa na mabo  hayo akaleta ghalika wakati wa Nuhu na kuchoma sodoma na gomora wakati wa Rutu.kwa namna nyingine inatupasa tujifunze kwamba uovu unaleta laana na mapigo mbalimbali katika jamii fulani.

 

*Namna  ambayo ni sahihi ya kufanya kusherehekea valentine kama siku nyingine alizotupa Mungu ni kupinga mambo yote ambayo yanaambatana na ubinafsi kama ufisadi,wizi na uongo.na kufanya mabo ambayo yanaleta na kujenga upendo kama siku nyingine yaani yale yanayoambatana na shukrani na namna yoyote ya kujali watu na jamii fulani(soma marko 12:31-32)

 

Aksante santa kwa kusoma walaka huu,Mungu akubariki uweze kuyatenda maneno haya na upate baraka katika namna ya ajabu.Jordan J.K MwaisakaEntreprenuer & Humanitarian

 

Note:Sikuandika walaka huu ili niweze kutambulika katika nafsi ya mtu au kuwa maarufu,bali ni namna ambayo nimepata msukumo wa kuweza kufikisha ujumbe ambao naona ni sahihi na yakinifu ili kulinda na kuokoa ili kumpa Mungu utukufu kwa sababu sisi sote ni kazi ya Mikono yake.Maswali maoni unaweza fanya comment hapo chini. 

Mwandishi wa makala hii anajulikana kwa jina la
Jordan Mwaisaka

No comments:

Post a Comment