Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu
mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango
naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa
mambo.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za
kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi
(nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na
kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu
ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi
tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote
wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali
ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati
huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa
wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka
kwenye masoko ya kimataifa.
Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu
wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo
tofauti na waliokosa elimu hiyo.
Kwa wana... wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.
Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa
business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza
starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale
unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya
kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye
maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati
isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi
Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana
kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri
sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna
soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa,
nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote
vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.
Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha
kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa
mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii
ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa
na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials
baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake.
Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na
interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye
assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga
tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na
mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya
kushika pesa kubwa.
Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na
kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.
Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha
kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza
kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona
Ahsanteni sana....
sOURCE: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-biashara-na-uchumi/39210-project-funding-sources.html
No comments:
Post a Comment