Mabingwa wa soka nchini timu ya Young African Sports Club almaarufu kama Yanga itatelemka dimbani siku ya Jumamosi kuivaa timu ya soka ya Komorozine de Domoni ya Visiwa vya Comoro katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika. Mechi hii inatarajiwa kupigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inarudi katika dimba hilo ikiwa ni siku chach tu baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 katika dimba hilo ilipopambana na timu ya Mbeya City. Hata hivyo mabingwa hawa wa soka hapa nchini wanaingia wakiwa na imani kubwa ya ushindi huku kukiwa na tetesi za kurudishwa kwa mshambuliaji wao toka Uganda Emmanuel Okwi.
Okwi ameonekana akiwa na wachezaji wenzie mazoezini na kuna taarifa kuwa jina lake litaidhinishwa na Shirikisho la Soka barani Afrika kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani. Kama kweli Okwi ataidhinishwa na CAF kuichezea Yanga basi timu hii itaimalika kwa kiasi kikubwa kwani uwezo wa Emmanuel Okwi si wa kutiliwa shaka hata kidogo.
Viingilio vya mchezo huo wa jumamosi ni:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
Aidha tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi (ijumaa) katika vituo vifuatavyo:
Makao Makuu - Young Africans SC
Kariakoo - Sokoni
Shule ya Sekondari Benjamini - Uhuru
Mwenge - Stand
Oil Com - Ubungo
Steers - Mtaa wa Samora
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI YANGA
No comments:
Post a Comment