Friday, 17 January 2014

HII TABIA WANAYO VIONGOZI WENGI TU.....POLE SANA KIONGOZI WANGU.

Katika kitabu changu kinachoitwa UTANI WA SERIKALI NA WANANCHI kuna chapter nimeandika inaitwa MKATABA WA MGOMBEA NA WANANCHI...Hebu soma utangulizi wake kisha angalia tukio lililo mkuta huyu Kiongozi wa nchi upande wa jimbo la uchaguzi na tabia hii si peke yake wapo wengi wa aina hiyo  tunawajua lakini tunalindana japo inatuuma sana, huyu binti kafungua mlango kwa wafanyakazi kuacha kuonewa; Sasa soma utangulizi wa chapter ya kitabu changu:
 
 

Mkataba ni makubaliano baina ya pande mbili juu ya jambo fulani linalohitajika kufanyika, na kila upande huridhika na makubaliano na asiwepo hata mmoja wa kumlaumu mwenzake maana maamuzi yalikwisha fikiwa. Historia ya Tanzania inaonesha huwa tuna mikataba bubu, upande mmoja ukionekana dhaifu kwasababu ya shida na umaskini. Kitu kinacho fanya wananchi kukubali kuingia mikataba wasiyojua faida yake wala hasara yake. Leo hii Tanzania kila nyumba ya kupanga ina bei yake na wapangaji hawalalamiki kutokana na shida ya upatikanaji wa vyumba, mikataba mibovu ya madini na mikataba ya ahadi na maneno matamu isiyo na maandishi kutoka kwa viongozi wetu.

 

Leo hii watanzania wamekuwa wakiumia sana na kukandamizwa na viongozi waliowachagua ili wa waongoze ama kwa kuteuliwa au kwa kupigiwa kura. Kila chaguzi zinapokaribia, hasa wakati wa kampeni wagombea wamekuwa wakitoa ahadi nzuri na tamu tena za kuridhisha, tatizo wakisha pata hizo nafasi walizokuwa wanataka, husahau ahadi zote walizoahidi na kugeuka wafalme.

 

Sasa turudi kwenye stori yetu hapo chini kama ilivyotufikia katika chanzo kimoja cha habari;
 
 
MH. MAHANGA ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKIUKA SHERIA ZA AJIRA.

 .Msaidizi wake wa ofisi ya Bunge afanya kazi miaka kumi chini yake bila mkataba
.Baada ya miaka kumi amlipa mafao ya laki mbili tu.
.Dada alalama kwamba Naibu Waziri alimtaka kimapenzi akakataa..soma zaidi hapa >>
http://bit.ly/1dWGhFl

No comments:

Post a Comment