Matembezi ya amani siku ya Pasaka wilayani kahama mwaka jana 2014 yaliyosababisha kushuka kwa gharama za matibabu hospitali ya wilaya kikao cha leo. |
Leo tarehe 17/01/2014 Baraza la madiwani wilayani kahama
katika kikao chake cha bajeti limeungana na chama cha NCCR-Mageuzi kwa kukubali
mapendekezo ya kushusha malipo ya hospitali ya wilaya kutoka Shilingi 3000/=
mpaka Shilingi 1000/=. Aidha madiwani hao baada ya kikao waliwaomba viongozi wa
NCCR-Mageuzi hasa katibu aliyekuwa kikaoni hapo kuwa wasisite kuibua hoja za
msingi. Ikumbukwe kuwa mwezi wa pili mwaka jana 2013 Chama cha NCCR-Mageuzi
kilikuwa na ziara ya Opersheni UZALENDO iliyokuwa ikiongozwa na katibu mwenezi
wa vijana Taifa ndugu Deogratius Kisandu ajenda kuu ilikuwa ni kupunguza
gharama za malipo hospitali.
Pia swala hilo liliendelea kuzungumzwa mwezi Desemba 2013 katika uzinduzi wa kitabu cha
Utani wa Serikali na Wananchi hapa wilayani kahama. Leo madiwani wote wa CCM,
CHADEMA, CUF na TLP wameendelea kusema tunakubali changamoto za kila aina na
tutaendelea kuungana na chama cha NCCR-Mageuzi katika hoja zake ili kuboresha
wilaya yetu. hata hivyo Gharama ya sh.1000/= itaanza rasmi tarehe 1/7/2014.
Mytake; AKSANTENI
SANA MADIWANI, MWENYEKITI WA HALMASHAURI, MKURUGENZI NA MKUU WA WILAYA KWA
KUONA UMHIMU WA KUFANYA HIVYO NA MUNGU AWABARIKI SANA. PAMOJA TUTASHINDA.
No comments:
Post a Comment