Tuesday, 14 January 2014

Mungu hamtupi mja wake. Godfrey Mambo anena yaliyo moyoni mwake

Ndugu Godfrey Mambo akiwa na mtoto siku ya walemavu kimataifa , ni jambo zuri na la kheri kuwajulia hali watoto walio katika nyumba za vituo vya kulea watoto yatima kwani Mungu hupenda zaidi binadamu wafanye hivyo, ndugu Mambo akiongea na Blogu ya Mwafrika amesema yuko mbioni kuanzisha Charity Center baada ya kuumizwa moyo sana na kupata huruma kubwa sana ya kuwasaidia watoto waliosahauliwa.     

Pia kaka Godfrey katika ukurasa wake wa Sura ya Kitabu kaandika hivi:
 
December 7, 2013 · Edited ·

Huyu nilifanikiwa kuongea nae... Anaitwa Suleiman anaishi Kigamboni lakini amesimama shule kwa muda wa mwaka sasa kwa sababu ya kukosa ada ambayo kwa Mwaka ni laki 5. Anapenda kuwa Mchungaji na anapenda Mathematics, English na Science.

Mbele yako Nyuma yake.

Sikia sauti yake kuwa Msaada wake.
 

Blogu ya Mwafrika inampongeza ndugu Mambo kwa kuonesha njia ya kujali watoto na Mungu akubariki sana.

No comments:

Post a Comment