Tuesday, 14 January 2014

HUU NDIO UKWELI WANGU KUHUSU CHADEMA

Naandika makala hii(Mimi Deogratius Kisandu)kwa Uchungu na furaha kubwa.Kuanzia miaka ya 2009-2012 vijana wengi waliokuwa Vyuoni waliijenga sana Chadema ikiwemo kuanzishwa kwa asasi ya CHASO waanzilishi wakiwa ni Deogratius Kisandu na Juliana Shonza na wengineo lakini pia kuliibuka vijana waliokuwa vyuoni na waliomaliza kipindi cha mwaka 2010 na kujitokeza kugombea nafasi za ubunge na udiwani wengine walipata na wengine hawakupata ambao ni Mtela Mwampamba, Deogratius Kisandu, David Silinde, Habib Mchange,Felix Mkosamali,Moses Machali, Chagulani Adam na wengine wengi. Kipindi hiki vijana walijitoa sana kujenga chama tena kwa kutumia nguvu zao mfukoni na ndipo vijana mihemko walipojitokeza wanaoamini kila kitu ni sawa. Lakini tija yao haikuonekana wengine walifukuzwa na wengine waliondoka wenyewe na wengine walibaki. Kiukweli wakati mwingine hutakiwi kulaumu kwa yaliyotokea ila ni kumshukru Mungu kwa kukuonesha njia nyingine ya kufikia malengo yako na kutimiza hata yale ambayo hukufikiria kuyatimiza ili kutimiza wajibu wa kumtumikia Mungu kama kiongozi.

Ikumbukwe kuwa nilikuwa mwenyekiti wa CHASO-Sekomu, Katibu wa Chadema(w)Lushoto, katibu wa BAVICHA(m) Tanga, mjumbe wa kamati tendaji wa BAVICHA. Nimezitumikia nafasi hizo kwa uaminifu na kwa nguvu zangu mwenyewe(akili, fedha na rasilimali nyinginezo zilizokuwa ndani ya uwezo wangu).

Namkumbuka Mbunge wa arusha mjini kaka yangu Godbless Lema alivyokuwa ananipa ujasiri sana hasa kipindi nilipokuwa nimepewa barua ya kujibu mashitaka ya kwanini nimemleta Lema wilayani Lushoto hasa barua hiyo iliibua mambo mengi sana ikiwa na mitego ya kila namna ili nifukuzwe chuo, japo vijana waliokuwa wanasoma sheria chuoni kwetu walinisaidia sana huku lema akinitia ujasiri wakutokuogopa na mwisho wa siku nilishinda Dhuluma na kufanikiwa kuhitimu chuo na hata Mkuu wa Chuo siku ya kupata cheti alinipongeza sana kwa ujasiri wangu na kuniambia angekuwa mwingine angekuwa kishaacha na chuo ila Mungu anampango nawe, timiza wajibu wako.

Makamu mkuu wa chuo mpya aliyeletwa kipindi tunaelekea kuhitimu chuo ndugu Molleli alipopewa taarifa kuhusu mimi mambo yalikuwa hivi; niliandika waraka wa kuwashukukru walimu wangu wote kwa nifundisha na kuwaahidi nitakwenda kufanya siasa safi kama ambavyo walikuwa wakiniasa mara kwa mara, makamu mkuu wa chuo nilipofika ofisini kwake akasoma waraka huo na kuniambia" Umesoma mpaka umehitimu chuo japo kwa vizingiti vingi na kushauri usikubali kufanya siasa za mabavu na siasa za kulaumu bila suluhu utajikuta unapoteza muda wako bure, bali fanya siasa za kubadilisha fikra kwa mlengo wa kidiplomasia na ukifanya hivyo hutaumia bali utaheshimika zaidi......" ni furaha kwangu japo leo hii wapo ambao wanasema nimeishiwa kumbe nimebadilika kimfumo na kisiasa.

Namshukru Mungu kwasasa nipo katika chama cha NCCR-Mageuzi tukifanya yetu kwa pamoja, kipindi kingine nitazungumza wajibu wangu kama mwana NCCR-Mageuzi.

TUJIKUMBUSHE TULIKOTOKA KATIKA PICHA.


Bango la uchaguzi mkuu wa ubunge 2010 jimbo la Lushoto ambapo ilitakiwa nigombee jimbo la nyumbani Kahama nikawekewa fitina ikanibidi nigombee ugenini sehemu niliyokuwa na soma chuo.


Deo Kisandu akihutubia mkutano nyumbani kwao wilayani kahama huku akizindua kitabu chake cha "UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU" katika viwanja vya Barcelona Septemba 2011.


Wanakahama wanampenda mtoto wao walikuwa wakijitokeza kwa wingi katika ziara ya uzinduzi wa kitabu "UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU" hii ni mwaka 2011.


Deo Kisandu akihutubia kina mama 2012

@Wilayani Kahama na vijana wenzangu , wengine wamehamia chama cha ADC na wengine NCCR-Mageuzi hapa ni  mwaka 2012.

Deo Kisandu wilayani Lushoto na Olle Milia, Ally Banange na Mawazo katika kujenga chama mwaka 2012 mapema tu walipotoka CCM kuja Chadema.

Olle Millia na Deo Kisandu wilayani Lushoto mwaka 2012.


Deo Kisandu na Mh.Mpendazoe wilayani Kahama mwaka 2011.

Vikao vya kujenga cha chuoni SEKOMU mwaka 2011.


Dr.Slaa alipomaliza kumnadi Deo Kisandu na Aron Mashumve mjini wa Mombo wilayani Korogwe katika picha ya pamoja.

Deo Kisandu na Henry Kileo katika uzinduzi wa tawi la chaso-Sekomu mwaka 2011.


Kisandu na kampeni za chama za ndani mwaka 2011 wakati nikigombea nafasi ya Mwenyekiti wa wa Taifa wa BAVICHA.

Katika harakati za pamoja mwaka 2012 mkoani Tanga.


Deo Kisandu, Benson Mramba, Nassary na Mh. lema katika uzinduzi wa Chaso-Sekomu mwaka 2011.

Mh.Lema na viongozi wilaya ya Lushoto mwaka 2011.

Hiki ndio kitabu kilichokuwa kikizinduliwa mwaka 2011.





DEO KISANDU-akifanya kampeni za kumnadi mgombe udiwani wa Chadema kata ya Funta jimbo la Bumbuli mwaka 2012.


Viongozi wapya wa baraza la uongozi mkoa wa Tanga wakithibitishwa na msimamizi wa uchaguzi Suzan Kiwanga(Mbunge)  mwaka 2011 akiwemo Deo Kisandu kama katibu wa BAVICHA.

No comments:

Post a Comment