Tuesday, 21 January 2014

HUYU NDIO MWANZILISHI WA CHAMA KIPYA CHA SIASA.....YEYE ASEMA WANANISINGIZIA.

Grayson Nyakarungu

Tangu miaka ya 1992 uruhusiwe mfumo wa vyama vingi kumekuwepo vyama vyenye mfumo wa aina moja wa uendeshaji majukumu yao. Tulitegemea kuona kutatokea vyama vyenye mfumo wa kitofauti kabisa na mfumo wa vyama vingine lakini hakuna tofauti wa kimfumo.

Watanzania tulitegemea kutakuwa na vyama ambavyo vitahutubia maendeleo na namna ya kuwakwamua kiuchumi vijana badala ya kupiga kelele za lawama bila kutoa suluhu ya matatizo yanayopigiwa kelele.

Mwaka huu wa 2014 kumetokea vyama kupewa usajili wamuda ikiwemo chama cha ACT. Blogu ya Mwafrika ilianza kumtafuta kijana machachari katika siasa za Tanzania Grayson Nyakarungu ambaye amekuwa akihusishwa na kuanzishwa kwa chama kinachoitwa AACT, akiongea kwa njia ya simu na Blogu ya Mwafrika, Nyakarungu amekanusha na kusema kwanza hakuna chama kinachoitwa AACT kama wanavyomtuhumu bali yeye anachojua kuna chama kinaitwa ACT kilichopata usajili wa muda na hata hivyo pia hahusiki katika hicho chama nawala hawafahamu hata hao viongozi wake.

Hata hivyo Blogu ya Mwafrika inawapongeza walioanzisha vyama kwani ni haki yao kikatiba.

No comments:

Post a Comment