Monday, 20 January 2014
WAKILI WA ZITTO ANENA UKWELI KUWATETEA VIONGOZI WA CHAMA CHAKE.
Diwani wa kata ya Mabogini Alberto Msando na Wakili kijana msomi ambaye amekuwa na mvuto mkubwa hivi karibuni hasa katika kesi ya kumtetea Mbunge wa Kigoma Kaskazini ( Mh. Zitto Kabwe). Hivi karibuni alikutana na changamoto ya maswali mengi kutoka kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga waliotaka kujua kuhusu yeye na hatima yake katika chama. Mh. Msando katika mahojiano hayo alikuwa muwazi sana na kujikuta akiwafariji wana Shinyanga kupitia JUKWAA LA SHINYANGA(Whatup); Wananchi walitaka kujua kama kuna viongozi wengine aliwahi kuwatetea na Msando alitoa majibu kama ifatavyo:
"Zitto ni mtu ambaye namtetea kwasababu naamini kwamba haki haitendeki. Gharama zangu nazibeba mwenyewe kama ambavyo siku zote nimekuwa na zibeba ninapowatetea viongozi wengine wa chama. Nimemtetea Mh. Mbowe na Mh. Ndesamburo kwenye kesi zao za Ubunge Moshi kwa gharama zangu. Nimemtetea Mh. Nassary bila yeye kulipa chochote. Nimewatetea viongozi na wananchama kesi za maandamano Arusha pamoja na wakili Kimomogoro bila kulipwa chochote. Nimemtetea Mh. Mbowe hai kesi ya jinai kwamba alimpiga kibao mwanaCCM bila kudai malipo."
Itaendelea...........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment