ILIVYOKUWA JANA.
Nafasi ya katibu Mkuu ilikuwa na wagombea watatu akiwemo mwananmke mmoja Bi. rehema lakini ushindani mkubwa ulikuwa kwa Katibu Mkuu aliyekuwa anamaliza mda wake Samwel Ruhuza na Naibu wake Mosena Nyambabe.
Kutokana na mchuano huo ulivyokuwa mkali sana na kuonekana huenda ukakigawa chama ili bidi dakika za mwisho Samwel Ruhuza aombe kujitoa ili kuepusha mpasuko ndani ya chama, Hivyo nafasi ya katibu mkuu alibaki Nyambabe na Mama Rehema Kahangwa, japo Nyambabe alishinda kwa kishindo lakini Bi Rehema alionekana kuwa kivutio kwa wajumbe kwa umahiri wake wa kuwasilisha hoja yake na hasa kutokana na jinsia yake. Hivyo tume ya uchaguzi ilimtangaza MOSENA NYAMBABE KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA TAIFA WA NCCR-MAGEUZI.
KATIBU MKUU TAIFA MTEULE NCCR-MAGEUZI.(MOSENA NYAMBABE) |
UPANDE WA NAIBU KATIBU MKUU
Hapa napo kulikuwa na tifutifu la watu watatu, Faustin Sungura, Ndugu Martin na Moses Machali (mbunge), kiukweli uchaguzi huu ulikuwa umejaa jazba sana ya wahusika, Ndugu Martin alijitoa mapema sana na wakabaki wagombea wawili. Dakika za mwisho kabisa Faustin Sungura alijinadi na kuanza kulia kwa hujuma alizofanyiwa katika uchaguzi huo na akaamua kujitoa kwenye nafasi hiyo na hivyo Machali kupita bila kupingwa. Hivyo tume ilimtangaza Moses Machali kuwa Naibu Katibu Mkuu bara.
NAIBU KATIBU MKUU BARA (MOSES MACHALI) |
UPANDE WA ZANZIBAR
Huku nako kulikuwa na wagombea wa wawili ambapo Musa Komba aliendelea kuitetea nafasi yake nakufanikiwa kushinda na hivyo Tume ilimtangaza Musa Komba kuwa Naibu Katibu MKuu Zanzibar.
NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR (MUSA KOMBO) |
UPANDE WA MHASIBU.
Mariam Mwakingwe alipita bila kupingwa kwa nafasi yake lakini wajumbe walipiga kura ya Ndiyo au Hapana. Na hivyo tume ilimtangaza Mariam Mwakingwe kuwa MHAZINI wa Chama cha NCCR-Mageuzi.
MHASIBU TAIFA (MARIAM MWAKINGWE). |
Makamishina wa mikoa wa chama cha NCCR-Mageuzi wote walidhibitishwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu.
Blogu ya Mwafrika inawatakia kazi njema wateule wote kwa nafasi zao.
source: jamiiforum via link; http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/590284-nyambabe-awa-katibu-mkuu-ruhuza-ajitoa-nccrmageuzi-machali-awa-naibu.html
No comments:
Post a Comment