Haya ni makubwa na simadogo sana ila kwasababu siku zote unapotafuta haki yako lazima ikugharimu kwa namna yoyote ile, Mbunge wa jimbo la Nzenga Khamis Kigwangalah katika ukurasa wake wa facebook ameandika hivi, hebu ungana naye ewe msomaji wetu wa online:
Nimepokea taarifa kuwa Madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa 'mahakimu' hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang'anywe ka...di ya uanachama wa CCM! Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi Chama kinavyoendeshwa Nzega. Ninaamini Viongozi wakuu wa Chama wanafuatilia kwa ukaribu na watachukua hatua stahiki. Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko Chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo, na hakuna wa kuingilia kati na kusema 'no', basi sina haja ya kuendelea kupambana. Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena! Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa. Nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako.
No comments:
Post a Comment