Thursday, 30 January 2014

UHURU UKIZIDI SANA NI HATARI,,,,,JE NDIO TANZANIA TUNAYOITAKA? ONA HIKI KISA CHA WIZI HAPA....

Kitendo cha wananchi kujichukulia Sheria mkononi huku wengine wakishabikia ni hatari kwa Taifa linalolia Demokrasia, kama kila kitu tutafanya maamuzi huku tuna majeshi tuliyoyapa dhama hatutafika, huenda hii inatokea pale wananchi wanapo hisi mtuhumiwa ukimpeleka polisi ataachiwa huru. Lakini hebu tujipime tunatengeneza Tanzania ipi?

Hebu tujiulize utakuta mtu mwenyewe kibaka lakini kumbukeni kuna majizi ya EPA kama haya tungeweza kuyachoma moto basi hata hao vibaka wasingekuwepo maana mtaji wao unatumiwa na MAFISADI. Kweli wanaoiba kwa kalamu hawa dhuliki ila wanaoiba kwa vitendo hayo ndo madhara yake. Blogu ya Mwafrika ina laani aina hii ya mauaji. UTU wa Mtanzania ni gharama yetu wote.

MWIZI ACHOMWA HUKO KAGONGWA KAHAMA MCHANA HUU,TAZAMA PICHA HAPA

 
Wananchi wakishuhudia mwili wa mtu anayedaiwa kuwa ni mwizi ulivyochomwa moto katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga mchana huu-----

No comments:

Post a Comment