Wednesday, 15 January 2014

USIJIFANYE WEWE NDIO UNA MAWAZO MAZURI KULIKO WENZAKO......ACHA NAWENZAKO WATOE MAWAZO YAO.....MBONA WEWE HUTAKI KUWASIKILIZA WENZAKO,,,,,,Twende tukadodose sasa

Blogu ya Mwafrika inaleta mjadala mpya tena wa Ukinzani katika mawazo na fikra huru........ona hapa jinsi wasiokubali mawazo ya wenzao wanavyoumbuliwa na Kiongozi mkuu wa kwanza wa Taifa letu Mwl. JK-Nyerere.....Mzeee anatiririka sasa:


“Kuna mambo mawili ya lazima katika demokrasia; ukiyakosa hayo demokrasia hakuna.  La kwanza; ni kwamba kila mtu lazima aweze kusema kwa uhuru kabisa, na maneno ya kila mtu lazima yasikilizwe.  

“Hata kama mawazo ya mtu huyu hayapendwi kiasi gani, au walio wengi wanamdhania amepotoka kiasi gani, si kitu.  Kama mtu anapendwa kwa wema wake, au hapendwi kwa visa vyake, hayo yote si kitu.

“Kila Mtanzania, kila mtu kijijini, kila mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya, kila Mbunge na kadhalika, lazima aweze kusema kwa uhuru bila hofu ya vitisho – ama katika mkutano ama nje ya mkutano.

“Watu wenye mawazo tofauti, hata wakiwa wachache, lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika majadiliano bila ya hofu ya kusumbuliwa; mawazo yao na yashindwe katika hoja za majadiliano, siyo kwa vitisho au mabavu.

“Majadiliano yenyewe yatakayoleta uamuzi lazima yawape nafasi watu kusema kwa uhuru kabisa.  Hata baada ya kuamua jambo, watu wawe na uhuru kuendelea kulizungumza jambo hilo.
“Maana wale wachache wenye mawazo tofauti lazima wafahamu kuwa kama wanayo mawazo yenye maana, na kama wakiyaeleza mawazo hayo vizuri, wanaweza kubadili mawazo ya wengine walio wengi.

“Kadhalika wale walio wengi lazima wawe tayari kuyashikilia mawazo yao mpaka wale wachache waridhike kuwa uamuzi uliofanywa juu ya jambo lile ulikuwa sawa.

“Majadiliano lazima yaruhusiwe kuendelea, kwa uhuru kabisa.  Hiyo ni sehemu ya maana ya uhuru wa mtu binafsi.” HIZI NDIO NUKUU ZA MWALIMU NYERERE.

J.K.Nyerere, Binadamu na Maendeleo, 1974.

No comments:

Post a Comment