Wednesday, 15 January 2014

Walimu waliotoa maoni kikao cha NAIBU WAZIRI Aggrey Mwanri wasimamishwa Kazi na Mkurugenzi.

     

Tumeiona mahala furani, kama ni kweli basi walimu wenyewe waliopewa barua hawajitambui, kwani katiba ya nchi Ibara ya 18 inampa mtu uhuru wa kujieleza, wadau wa blogu ya Mwafrika wanaamini kuwa Katiba ya nchi ndio kiongozi mama lakini Waziri mwenye dhamana yupo kama taarifa ni za kweli tunaimani litashughulikiwa. Hebu msomaji wetu dodosa na wewe taarifa hii kama ni ya ukweli au laa!

 

Walimu waliotoa maoni kikao cha NAIBU WAZIRI Aggrey Mwanri wasimamishwa Kazi na Mkurugenzi.

Mkurugenzi wa Meatu John Wanga mkoani Simiyu amemsimamisha kazi kwa barua mwl Baruti wa sm Mwanyahina aliyewakilisha walimu kutoa kero mbalimbali za walimu wilayani humo kwenye kikao cha ndani na Aggrey Mwanri mpaka atakaposibitisha tuhuma zote alizotoa.

Tuhuma alizozitaja ni

Walimu kutolipwa fedha zao za likizo na Uhamisho na Mafaili yao kuandikwa Paid. Na wakiambiwa pesa hakuna Nasisitiza tuhuma hizi ni ukweli mtupu majina ya walimu hao tunayo.

Walimu kucheleweshewa fedha za likizo hadi likizo imeisha na fedha kutumika kwa mambo mengine.

Kuna mabadiliko makupwa ya ulipwaji wa stahili mbalimbali za walimu toka mkurugenzi mpya ahamie.

Pili walimu walionywa kabla kutochangia wala kuongea lolote kwenye kikao hicho la sivyo chamoto watakiona na limekuwa ni Rungu kuzuia Walimu kutohudhuria kikao chao na Mbunge wao Meshaki Opulukwa alichopanga kifanyike tare 23 januari ili kusikiliza kero zao
Pia rungu la mkurugenzi limemkuta walimu kadhaa kwa kuhamishiwa mazingira magumu huku kuna madai makubwa ya uhamisho ambayo hayajalipwa.

Niliandika uzi wa ziara ya Jk wilaya ya MEATU kutumia fedha zote za walimu ukafutwa.
Je alinayoyafanya mkurugenzi ni Maagizo ya naibu waziri alipokuwa anaondoka?.

Taarifa nilizozipata sasa ni kwamba mwalimu aliitwa na mkurugenzi leo kwa njia ya simu na KUHOJIWA NI LINI AMEPEWA CHEO CHA USEMAJI WA HALMASHAURI.
Last edited by William Mshumbusi; Yesterday at 19:02.
TUJITEGEMEE likes this. SOURCE: JamiiForums.com

No comments:

Post a Comment