Sunday, 2 February 2014
DKT.CHENI AFUNGUKA WASANII KUTOJITOKEZA MSIBA WA VICTOR WA BONGOMUVU KULE KAHAMA,waipa pole familia
Yafuatayo ni mahojiana ya leo asubuhu baina ya Dkt.cheni na Blogu ya Mwafrika juu ya nini kilichojiri kwa waasanii baada ya msanii mwenzao kujinyonga na nini ushirikiano wao kwa msanii mwenzao katika mazishi kule wilayani kahama. Pata interview zaidi ilivyokuwa na Bloga wetu:
Blogu ya Mwafrika: DKT.CHENI unafikiri kwa nini msanii mwenzenu Victor wa Bongo Muvu kajinyonga?
DKT.CHENI: Ndugu kwa kweli tukio hilo ni la kusikitisha sana na haifahamiki mpaka sasa chanzo ni nini, maana mimi nimesoma tu magazetini kuwa walimaliza kufanya shooting yake inayoitwa My family kama sikosei na akawalipa wenzake pesa walizokuwa wamekubaliana na ndipo akajitundika. Hii huenda ni msongo wa mawazo aliokuwa nao msanii mwenzetu na kufikia kufanya maamuzi magumu kama yale ni challenge sana kwetu kama wasanii.
Blogu ya Mwafrika: Je kuna msanii mwingine alishawahi kufanya tukio kama hilo la kijasiri kujitoa uhai?
DKT.CHENI: Hapana na haijawahi kutokea hiii ndio ya kufungulia mwaka.
Blogu ya Mwafrika: Kuna uhusiano gani kati ya filamu yake na maisha yake?
DKT.CHENI: Kwa mtazamo wangu ukisoma magazetini filamu hiyo wanasema inakipengele cha kujinyonga ambapo mhusika alikuwa ndio muigizaji katika script hiyo, may be inaweza kuwa msanii mwenzetu alikuwa na mgogoro wa kifamilia na akaona baada ya shooting afanye hivyo na hii nafikiri tusubiri muvu yenyewe itoke tutakapoiona ndio tutajua ukweli wa kisaikolojia na wachambuzi wanaweza kuelewa zaidi kama ilikuwa ni maisha maana wakati mwingine huwa tunaigiza maisha tuliyopitia.
Blogu ya Mwafrika: Mbona wasanii maarufu kama wewe, lulu, wema na wengine hamjashiriki mazishi kule Kahama zaidi ya Koba na wengine ambao ni chipukizi?
DKT.CHENI: Kaka asikwambie mtu, wasanii tuna maisha magumu sana ila majina ni makubwa, hakuna msanii ambaye bajeti yake inaweza kumruhusu kwenda kahama kwa mazishi na kurudi pamoja na kulala na kula, ndio maana unaona Msanii mwenzetu Kanumba alizikwa Dar ili wasanii tuweze kushiriki, vinginevyo ni ngumu sana.
Blogu ya Mwafrika: Unanini sasa cha kusema kwa familia ya msanii mwenzenu?
DKT.CHENI: Tunawapa pole wanafamilia wote na wanakahama wote na sisi tutajipanga kama wasanii kwa kuandaa rambirambi zetu. MUNGU AILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MSANII MWENZETU VICTOR P. MAKULA.
Blogu ya Mawafrika: Tunakushukru kwa ushirikiano wako kaka Cheni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment