Tuesday, 4 February 2014

Kuuliza Multiple Choice Question katika University Exams: Tunapima nini?

MAONI YA MDAU WETU WA LEO:

Nimekutana na karatasi ya Maswali ya Mtihani uliopita mwaka wa 3 (Final Year) pale UDSM una maswali ya multiple choice kama 20 hivi na kila swali lina marks 1, hivyo mtu akipata maswali yote hata kwa ku-guess tu ana marks 20 tayari kati ya 60 anazotakiwa kupata katika University Exam (UE). Swali langu ni kwamba, wa level ya Chuo Kikuu (University) tena Mwaka wa 3 anayepewa multiple choice kweli tunaanda wataalamu wa aina gani?

Rai Yangu:
Ningeshauri vyuo vikuu vibadili mtindo huu wa kutunga maswali (Multiple Choice) maana unavutia (encourage) kubahatisha (guessing) bila kufikirisha akili ya mwanafunzi.

Najua hapa watakuja watu kuutetea, ooh idadi ya wanafunzi wamekuwa wengi ndo maana lecturers wanatunga multiple choice questions ili iwe rahisi kusahihisha lakini sababu hiyo tu haitoshi kuharibu wanachuo hawa ambao baada ya kumaliza hapo, wanaenda kupambana na wasomi wa Kenya, Uganda, Afrika Kusini & dunia nzima.


Je wewe msomaji wetu una maaoni gani juu ya hilo?

1 comment:

  1. Katika nasharia za elimu ya ualimu, maswali kama ya kuchagua (multiple choices) na mengineyo kama ya kuoanisha (matching items) hutumika kupima kumbukumbu na uelewa wa mada husika.. ni maswali mazuri sana katika mtihani hasa kama nia ni kupima specifics katika uelewa... Uelewa na ujuzi Knowledge and understanding ndio ngazi za awali za bloom of taxonomy upande wa cognitive domain...

    ReplyDelete