Thursday, 6 February 2014

SERIKALI IUNDE SHERIA YA KUFUMANIA.....zaidi ingia hapa.



 Kumekuwepo na wimbi la muda mrefu sasa ambapo wanaume au wanawake kufumania wenza wao wakiwasaliti, na haya yote wapo waliojichukulia sheria mkononi na ikawagharimu, wapo waliopoteza maisha sababu ya kusalitiwa, wapo wanaokula maisha sababu ya kuumiza wenzao. 

Kesi za ufumanizi hata zikipelekwa polisi mara nyingi huwa hazipewi kipaumbele sana na huambiwa myamalize wenyewe. Kwa kuwa ndoa ni gharama kwa maana ya uaminifu ni budi sasa serikali ikatunga sheria ya Ufumanizi ili kulinda thamani ya ndoa na kuepuka watu kujichukulia sheria mkononi. Haya ni maoni ambayo Blogu ya Mwafrika bado inaendelea kuyatafutia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment