Kampeni zawaunganisha Maige, Lembeli
Maige aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Lembeli ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ni mahasimu wakubwa kisiasa licha ya wote kutoka wilaya moja ya Kahama.
Waziri huyo wa zamani, anamshutumu Lembeli kwa kuandika ripoti yenye upotoshwaji mwaka 2012 na kumfanya aondolewe katika nafasi yake ya uwaziri.
Kwa sababu hiyo, kitendo cha Maige kufika kwenye jimbo la hasimu wake na kufanya kampeni hizo, kiliwashangaza baadhi ya wafuasi wa CCM kwa kuwa ni mara ya kwanza tangu alipoondolewa kwenye uwaziri kufika Kahama kwa shughuli za kisiasa.
Katika kampeni hizo, Maige alimuuunga mkono Lembeli kwa juhudi zake za kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo na kuwashauri wakazi wa Ubagwe wamchague Majogolo ili ashirikiane na mbunge wao kuharakisha maendeleo kauli iliyozungumzwa pia na Lembeli kwa nyakati tofauti.
Uchaguzi mdogo utafanyika Februari 9 baada ya aliyekuwa Diwani wa Ubagwe, Robert Mdula kufariki dunia mwaka jana.
Vyama vingine vinavyoshiriki na wagombea wao kwenye mabano ni CHADEMA (Adam Ngoma) na Tadea (Machibya Lubinza).
Chanzo: TanzaniaDaima online.
No comments:
Post a Comment